AUDIO Gospel Lyrics Music VIDEO

Ambassadors Of Christ – Yatupasa Kushukuru

Lyrics

Mtu mmoja alistaajabu sana niliposema nitamshukuru Mungu
Baada ya matatizo mengi kunipata akili yangu ikampa wasiwasi
Kwa kweli nami, ilinigharimu, kujijulisha inipasavyo
Ila baada ya muda nikaona yapo mengi ya kunifanya nimshukuru Mungu

Yako mengi, hayajakwisha yatubidhishayo tumshukuru Mungu wetu
Japo twapita majaribu mengi bado, yapo mengi ya kushukuriwa
He ee jiunge nasi, tulisisitize jambo hili la muhimu
Yale yote tujiulizayo mioyoni majibu anayo Mungu wetu

Ambassadors of Christ tuashukuru lakini kwa wengi hatueleweki
kutokana na mambo ya yaliotupata ili kushukuru si jambo la busara
Lakini ndugu, ukitulia, nakujiuliza ya ajali ile
Tungeweza kuangamia wote kwa pamoja asiwepo hata mmoja wa kusimulia

Yako mengi, hayajakwisha yatubidhishayo tumshukuru Mungu wetu
Japo twapita majaribu mengi bado, yapo mengi ya kushukuriwa
He ee jiunge nasi, tulisisitize jambo hili la muhimu
Yale yote tujiulizayo mioyoni majibu anayo Mungu wetu

Majaribu kama haya yalikuweko hata kwenye siku za mababu zetu
Ila kwa yote walikuwepo mashujaa walioweza kuitetea imani yao
Tuwake Mungu, wakati wote, kwa yote hatujitegemei
Tukiwa hai tukiwa mauti tuwake tujualo ni moja kushukuru

Yako mengi, hayajakwisha yatubidhishayo tumshukuru Mungu wetu
Japo twapita majaribu mengi bado, yapo mengi ya kushukuriwa
He ee jiunge nasi, tulisisitize jambo hili la muhimu
Yale yote tujiulizayo mioyoni majibu anayo Mungu wetu

He ee jiunge nasi, tulisisitize jambo hili la muhimu
Yale yote tujiulizayo mioyoni majibu anayo Mungu wetu

Translate to English

AUDIO Ambassadors Of Christ – Yatupasa Kushukuru MP3 DOWNLOAD

Leave a Comment