AUDIO Lyrics Music VIDEO

Harmonize – Nitaubeba 

Lyrics

Imagine uko jangwani umepotea
Mchana juani unatembea
Utokapo ni mbali uendapo ni mbali
Mara ngamia mbebaji akatokea


Na kukushusha mzigo uliokuelemea
Upate afadhali pole na safari
And thats why today
To me yote tisa ila kumi
Umeonesha maana ya upendo
Si kwa maneno bali kwa vitendo


Umeridhika na nilichonacho
Vya watu hutoleagi macho
Siku nikiwa sina twalala
Oooh baby twalala
Aaaah baby if I close my eyes


Mi namuomba Mungu akulinde
Na akusimamie we ndo
Pacha wangu mie

Eti siku hizi vipi mbona sikusikii tena
Sikusikii ukilia sikusikii ukisema


Niko busy na boo jamani nimeshasema
Niko busy na baby na msalaba wake

Nitaubeba, nitaubeba nitaubeba
Na ntafika nao kiume
Nitaubeba (iwe kwenye shida na raha)


Nitaubeba (ama kwenye shibe na njaa)
La kwako ndo langu my darling
Na ntafika nao kiume

Imagine hujifahamu
Umezimia umewekewa damu zinaingia
Bomba ikafunguka na huwezi hata nyanyuka
Mara dakitari wa zamu


Akaingia umepata fahamu unamwangalia
Machozi yanakuanguka unatamani funguka
And that’s why today to me
Yote tisa ila kumi unanifurahisha
Kwenye tendo
Au unipe penzi la magendo


Aaaah baby if I close my eyes
Mi namuomba Mungu akulinde
Na akusimamie we ndo pacha wangu mie

Eti siku hizi vipi mbona sikusikii tena
Sikusikii ukilia sikusikii ukisema
Niko busy na boo jamani nimeshasema


Niko busy na baby na msalaba wake

Nitaubeba, nitaubeba nitaubeba
Na ntafika nao kiume
Nitaubeba (iwe kwenye shida na raha)


Ntaubeba (ama kwenye shibe na njaa)
La kwako ndo langu my darling
Na ntafika nao kiume

Iwe kwenye shida na raha
Ama kwenye shibe na njaa
La kwako ndo langu my darling

Translate to English

Leave a Comment