MAKALA

Jinsi ya kupika Biryani tamu lenye ladha nzuri

Mahitaji

 • Vipande vya kuku kilo 1
 • Mchele wa basmati gramu 400 (unaweza kutumia mchele unaopenda)
 • Kitunguu maji 1
 • Nyanya zilokatwa 5
 • Vitunguu saumu punje 5
 • Pilipili za kijani 4
 • Mafuta ya kula vijiko vya chakula 4
 • Mdalasini vijiti 4
 • Hiliki 3-4
 • Tangawizi iliopondwa vijiko vya chakula 2
 • Majani ya nanaa yaliyokatwa kiganja 1
 • Binzari nyembamba kijiko cha chai 1
 • Chumvi kijiko cha chai 1
 • Manjano kijiko cha chai ½
 • Zaafarani kijiko cha chai ½ (si lazima)
 • Kotmiri iliyokatwa kikombe ¼

Matayarisho

Loweka mchele wa basmati kwenye maji na uweke pembeni kwa dakika 15 hadi 30 (kama hutumii mchele wa basmati basi utaangalia mwenyewe mchele unaotumia)

Maelekezo

 • Weka mafuta kwenye sufuria, yakipata moto kaanga kitunguu maji hadi view na rangi ya kahawia.
 • Twanga kwa pamoja binzari nyembamba, kitunguu swaumu, tangawizi, nusu ya pilipili na vijiti viwili vya mdalasini, kisha weka kwenye vitunguu ukaange pamoja kwa dakika tatu.
 • Tia nyanya na pika kwa dakika tano
 • Tia vipande vya kuku koroga, acha iwive kiasi cha dakika 10 hadi 15 na ikaukie
 • Weka pilipili zilobaki kotmiri na masala ya kuku. Pika rosti liwe zito.
 • Acha rosti na weka pembeni.
 • Chemsha maji kwa hiliki na mdalasini na chumvi kisha weka mchele lakini usiwive kabisa kwa dakika tano baada ya hapo mwaga maji.
 • Panga wali na masala.
 • Kwanza chemsha maji ½ kikombe katika sufuria utakayopikia biryani. Maji yakishachemka anza kuweka wali kisha rosti na malizia na wali. Kama una tumia zaafarani…
 • Zaafarani kawaida hurowekwa kwenye vijiko vyenye maziwa ya vugu vugu na kumwagilia kwa juu.
 • Weka moto mdogo kwa dakika 30. Baada ya hapo chakula chako kitakuwa tayari.

Leave a Comment