MAKALA

Jinsi ya kutengeneza keki nzuri iliyochambuka.

Keki hutengenezwa kutokana na unga wa ngano, mafuta, mayai na vikolezo mbalimbali. Kuna keki za aina mbalimbali kulingana na umbo, ukubwa, vikolezo nk.

Aina za keki pia hutegemea wakati (Ocassions) kwa mfano kuna keki za harusi.kumbukumbu ya kuzaliwa na zile za kawaida.

Keki hutengenezwa kutokana na unga wa ngano, siagi, sukari, baking powder na mayai, kadhalika vanilla na maziwa  na vikolezo vngine vinaweza kutumika.\

Unga wa ngano unaleta matokeo mazuri kwenye keki ni wenye protini nyingi(11-13%)  Kama ilivyo kwaa mkate keki  pia inaweza kutengenezwa kwa kuchanganya unga wa aina nyingine  kama muhogo, soya n.k. kutegemea na matakwa.

1 Kanuni za kiteknolojia zinazohusiana na utengenezaji wa keki

Sifa kubwa ya keki ni kuwa nyepesi, kuchambuka na kutokunata mdomoni wakati wa kula. Muundo wa wepesi wa keki hutokana na hewa nyingi iliyojazwa katika donge wakati wa kukoroga pamoja na viambaupishi vinavyosaidia  kazi hii. Ili kufanikisha hili  korogaji lazima uwe wa kuelekea upande mmoja.

2 Kazi ya Viambapishi

  • Sukari huongeza radha kwenye keki, uwezo wa kuhifadhi na huchangia  katika kuwezesha keki kuwa nyepesi
  • Siagi huongeza radha hasa baada y kuoka
  • Mayai: husaidia kuongeza na kuhifadhi hewa ndani ya donge  na hivyo keki kuwa nyepesi,. Pia huleta ladha nzuri ya keki bada ya kuokwa.

VIAMBAUPISHI:

  • Unga wa ngano 1kg
  • Sukari 0.4kg
  • Siagi 0.4kg
  • Mayai 10
  • Dawa ya kuokea (baking powder) vijiko vya chai 6
  • Vinvginevyo: maziwa, vanilla, chumvi-kidogo

3 VIFAA

  • Oven
  • Chekecheo
  • Mwiko
  • Mizan
  • Meza
  • Bakuli au mashine ya kuchanganyia
  • Vibati vya kuokea
  • Vifungashio

4 HATUA ZA UTEMGENEZAJI

  1. 1. Unga  :               Chagua unga mzuri unaofaa kwa keki. Pima kipimo kinachohitajka katika mizani. Chukua baking powder  na changanya vipimo  kama no. 3
  2. 2. Chekecha  : Chekecha ung a kwa kutumia  chekeche lenye matundu madogo madogo. (chekecha pamoja na baking powder)
  3. 3. Changanya: kilo moja ya unga weka 400g za siagi, sukari 400g, dawa ya kuumulia (baking powder)   vijiko vya chai 6-8, mayai 10,chumvi. Maziwa, vanilla kidogo
  4. 4. Changanya: sugua siagi na sukariiliyosagwa  mpaka itoe mapovu( creaming method), piga mayai mpaka yatoe povu ongeza kwenye mchanganyiko wa siagi na sukari polepole  huku ukikoroga mpaka vichanganyikane vizuri,changanya  unga na vikolezo vyote. Oneza maziwa au maji  ili kuweza kupata uji mzito.
  5. 5. Jaza; weka mchanga yiko kwenye vikopo au vikopo vya kuokea.
  6. 6. Oka: oka kwenye nyuzi joto 2250c-2500c kwa muda wa dakika10-15 ambayo keki zako zitakuwa na rangi ya  kahawia
  7. 7. Pooza:Panga kwenye waya/ chombo cha kupozea.
  8. 8. Funga: weka kwenye mifuko ya plastic na funga vizuri.

5 KUHIFADHI NA KUDUMISHA UBORA

Kudhibiti ubora na hatua za utengenezaji  ni kam kwenye biskuti. Keki iliyotengenezwa vizuri inaweza kukaa siku 5-7 bila kuharibika.

KUTENGENEZA KEKI KWA KUTUMIA UNGA WA MUHOGO;

  • Malighafi unga wa muhogo 500g na unga wa ngano 500g
  • Sukari 250g
  • Mafuta mazito(blue band) 400g
  • Baking powder 30g
  • Vanilla 15ml
  • Maziwa 300ml hadi 500ml
  • Mayai 10

Hatua za utengenezaji zinafanana kama ilivyo kwenye keki za ngano.

6 KUPAMBA KEKI

Upambaji wa keki ni uongezaji wa madoido ya aina mbalimbali ambayo huifanya keki ipeneze na kuvutia zaidi . Madoido hayo ni kama vile nyota, maua, na mengine mengine mengi kama maandishi ambayo yanaashiria tukio

Kupamba keki ni  sanaa imekuwa ikitumika kufanya matukio yafane  kama harusi, kumbukumbu ya kuzaliwa na uzinduzi n.k.

Mapambo ya keki hutengenezwa kwa kutumia sukari na siagi au mayai, rangi ya vyakula, ladha na aina yoyote ile yap ambo linaloweza kuwekwa kutegemeana na wakati. Hata hivyo mafanikio mazuri ya kupamba yatategemea vifaa vilivyotumika paoja na ufundi wa usanii wa mpambaji.

VIFAA:

  • Bakuli ya kukorogea mchanganyiko
  • Bakuli za kuchanganyia rangi kutegemea na idadi ya rangi zitakazotumika
  • Visu vyenye ubapa
  • Seti ya mashine ya kupambia
  • Mwiko na vijiko vya kukorogea
  • Sahani
  • Chanja za kuinulia keki iliyopambwa
  • Brashi
  • Kisu cha msumeno

7 Upambaji wa kutumia siagi

  • Viambaupishi
  • mafuta ya mgando(pride, kimbo n.k.)siagi 100g
  • Sukari iliyosagwa 800g
  • Maziwa au maji 20ml
  • Vanila 5ml

AU

UPAMBAJI WA KUTUMIA UTE WA YAI

Viambaupishi.

  • Ute wa yai 20ml
  • Sukari iliyosagwa 500g
  • maji ya limao 20ml
  • Vanila 3ml

Hatua za utengenezaji

Sugua  : Sugua mafuta na siagi, ongeza maji, sukari na vanila endelea kusugua mchanganyiko hadi uonekane kama krimu.

AU Sugua sukari na ute wa yai mpaka upate donge zito ongeza maji ya limao na vanila endelea kusugua hadi upate  mchanganyiko unaofanana na krimu nzito.

Tayarisha:   Tayarisha keki inayotakiwa kupambwa, kama keki haikulingana isawazishe kwa kukata sehemu zilizozidi, tumia kisu cha msumeno. Toa punje punje zilizobakia kwa kutumia brashi.

Unganisha: Unganisha vipande vya keki ili kupata ukubwa unaotakiwa. krimu ya keki iliyotengenezwa kwa kufuata hiyo hapo juu ndio itakayotumoka kama gundi kuunganisha vipande inapobidi kufanya hivyo. tumia kisu chenye ubapo kupaka krimu sehemu zitakazounganishwa. Unganisha sehemu zilizopakwa krimu upate keki moja itakayopambwa kulingana na ukubwa utaotaka.

Paka: Weka kiasi kikubwa cha krimu juu ya keki, sambaza krimu hiyo kwa kutumia ubapa  ukisukuma krimu inayozidi kuelekea sehemu za chini za keki pande zote .

Paka: Paka krimu sehemu za pembeni za keki kuifunika yote   fanya taratibu upande mmoja huku ukizungusha sahani, hakikisha krimu imekaa vizuri kutokana na matakwa.

Jaza: jaza krimu katika mashine pamba kufuatana na matakwa au tukio. Maandishi yanaweza kuwekwa maua katika rangi mbalimbali na yote yatafanywa kutokana na lengo la keki.

KUDHIBITI UBORA

Malighafi:

Sukari iwe iliyotengenezwa maalumu  kwa kazi hiyo ili kupata matokeo mazuri.

UTENGENEZAJI:

Krimu laini inarahisisha hatua ya kwanza ya kufunika keki ili kupata ulaini huo ongeza 10ml za maziwa( upambaji wa siagi) au 10ml juisi  ya limao (upambaji wa ute wa yai)

BIDHAA:

Upambaji wa kutumia siagi hufaa zaidi  katika nchi za baridi kwani katika joto kali siagi huyeyuka, hata hivyo keki iliyopambwa kwa njia hii huweza kutumika katika sehemu za joto kama tu itahifadhiwa katika friji na kutumika mara tu itolewapo.

Leave a Comment