MAANDALIZI
Unga wa ngano nusu
Sukari glasi ndogo nusu (1 ikiwa wewe ni mpenzi wa sukari)
Chumvi robo kijiko cha chai
Iliki punje 10 hivi
Custard kijiko kimoja cha chakula
Samli kijiko 1 cha kukulia
Tui la tunda la mnazi glasi ndogo 2
Hamira vijiko 2 vya kukulia
Baking powder kijiko 1 cha kukulia
Mafuta ya kupikia nusu lita

Chekecha unga kwa kutumia chungio kwenye chombo utacho kandia unga wako.
Chukua kikombe weka hamira, sukari vijiko 2, unga vijiko 2 na iache kwa dakika 5 mpaka ifure.
Chukua unga ulio uweka kwenye chombo chako,weka baking powder,chumvi,sukari,hiliki na custard kisha changanya vizuri.
Chukua hamira iliyoumuka changanya na unga wako kisha weka tui lako kidogo kidogo na uanze kuukanda.
Kanda unga wako kwa dakika 10 mpaka uwe laini kisha uuache kwa muda wa dakika 5.
Ongeza samli na uendelee kuukanda unga kisha uweke kwenye bakuli na uufunike ili usipitishe hewa uache tena kwa muda wa dakika 10.
Ukishaumuka kata madonge na uyasukume kwa kutumia unga mkavu upate duara kubwa kama chapati hivi, ila isiwe nene sana wala nyembamba sana. Kisha kata mandazi yako kwa umbo la pembe tatu ama upendavyo.
Yaache mandazi yako yaumuke kwa dakika zisizopungua 10 hivi.
Mimina mafuta kwenye karai yaache yapate moto kiasi kisha anza kuweka vipande vyako hatua kwa hatua.
Hakikisha mandazi hayawi mengi kwenye karai ili yaachane na uweze kuyageuza kwa urahisi.
Ili andazi liumuke vizuri wakati lipo katika karai, limwagie mafuta juu kwa kutumia mwiko wako, alafu ndio uligeuze baada ya kuumuka vizuri.
Andazi likiiva epua weka kwenye chujio au shashi kulichuja mafuta ya ziada.
Likipoa tayari kwa kula kwa chai, mchuzi wa nyama yoyote ile, mbaazi, maharage n.k.

Leave a Comment