AUDIO Lyrics VIDEO

NGUVU YA MSAMAHA BY AMBWENE MWASONGWE

lyrics

Alisikia minong’ono mtaani
Watu walikuwa wakiteta kuhusu yeye
Masikini huyu hakujijua
Alijiondokea
Akitikisa
Kichwa chake
Asante sana Bwana umenisaidia mabaya hayakunikuta Mimi

Kumbe maneno Yale yalikuwa yake
Ila bahati mbaya hakuyajua
Alipoyasikia alidhani mapya kumbe yalikuwa yanakwisha

Alipogundua yanamuhusu
Alihangaika ajitetee
Aliwalaumu sana
Rafiki zake kwa kujua wamenyamaza

Nyamaza usilie
Mungu atakusaidia
Hajawahi tupa mtu
Nawe hatakutupa

Yakamshinda kuvumilia
Mabaya Yale
Kila alipowaona wabaya wake moyo wake ulipasuka
Akapanda gari asijue aendako
Njia nzima alikuwa akiwaza
Kwa Nini baba yangu achukue mke wangu

Aliwalilia watoto wake
Ninawaacha mkiwa wadogo
Sikutamani niishi hivyo
Ila mama yenu kasababisha
Ninakwenda nikafie mbali
Ninasikitika hamtaniona
Nisameheni wanangu
Sitaki Babu yenu na mama yenu waone maiti yangu

Mwanangu unadhani ubaya huu
Uliotendewa
Unaweza kufutika kwa kuutoa uhai wako?
Je! Pia unadhani uchungu ulionao moyoni unaweza kufutika kwa kulipa KISASI?

Malaika wa Bwana walimfuata alikoenda
Kila alipojaribu kujiua Mara zote Hilo lilishindwa

Sauti ya Bwana ikasikika ikimwita
Rudi nyumbani ukawaombe msamaha baba yako na mke wako

Usiende kuwambia watoto wako
Ubaya wa mama yao uliotendewa
Usije mlaumu baba yako
Mbele ya macho yao walasikia

Mimi nakutuma
Nina kusudi ukifika ukawaangukie
Nataka nijitukuze kwa nguvu ya Msamaha nenda nipo nawe

Nyamaza usilie Mungu atakusaidia hajawahi tupa mtu nawe hatakutupa

Unajua Mungu unanionea wamenikosea hawakuniomba msamaha
Nilipoondoka waliniona, japo watoto wangu na mama yangu sikuwaaga

Iweje leo, Uniambie nirudi
Nikawaombe wao msamaha Tena?
Wakati wenyewe walipaswa kuniomba Msamaha

Ninajua moyo wako ulivyoumizwa mwanangu
Ndio maana nakutuma upone
Ninakutuma nenda kawaonyeshe nguvu ya Msamaha

Translate to English

AUDIO | Ambwene Mwasongwe – Nguvu ya Msamaha | Download Mp3 [New Song]

Leave a Comment